Tanzania,Kenya,Uganda katika historia CHAN 2025

 

Kenya, Uganda na Tanzania wataandaa pamoja Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN) ya mwaka 2025 Yatakayo anza  Februari 1-28, 2025,  mashindano ambayo yanahusisha wachezaji  kutoka  ligi  za ndani  ya nchi  pekee.

 Uthibitisho huo umetolewa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe,  mapema wiki katika ziara yake nchini Kenya iliyokuwa na lengo la kuona maandalizi ya viwanja  vitakavyotumiwa katika mashindano hayo ,ambapo  alitembelea viwanja vitatu vya kitaifa vya Kenya ambavyo vimepangwa kuwa wenyeji wa tukio hilo.

 "Sina shaka kwamba Kenya, Uganda na Tanzania wataandaa CHAN bora zaidi katika historia ya mashindano haya kwa sababu nimeona  jinsi serikali zilivyo tayari na zinavyofanya kazi kwa bidii ,ambayo inawapa kila mmoja fursa ya kuboresha miundombinu ya  kandanda na kuvutia maelfu ya wageni na kuimarisha utalii wao,”alisema Motsepe baada ya kuongoza mkutano wa kamati ya utendaji ya CAF.

Aidha Bw . Patrice Motsepe,ameongeza kuwa mashindano ya mataifa ya Afrika CHAN ni fursa nzuri ya wachezaji wa  Afrika inayokuza  washindi wajao wa AFCON .

 Itakuwa mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuwa mwenyeji wa mashindano ya kandanda ya kimataifa kwa timu za kitaifa CHAN na itakuwa maandalizi kwa mataifa hayo matatu kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) la mwaka 2027 Nchi tatu za Afrika Mashariki  kuanda mashindano ya CHAN itaongeza timu shiriki  hadi kufikia 19 kutoka za awali  18 huku Mechi za kufuzu  19  bora  zitaanza tarehe 25 Oktoba na kumalizika mwezi Desemba  2024 .

Bingwa wa mashindano yaliyopita 2023  ni Senegal ambayo alitwaa taji hilo  baada ya kuwashinda kwa penati  5-4 wenyeji Algeria,Moroko na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kila moja imewahi  kushinda taji la Chan mara mbili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.

 Mwandishi;Harieth Kamugisha

mhariri;Ellukagha Kyusa


 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kenya, Uganda and Tanzania to co-host 2025 CHAN

18th September 2024

September 18 – Kenya, Uganda and Tanzania will co-host the 2025 Africa Nations Championship (CHAN) in February 1-28, 2025, the African tournament that sees nations select players from their domestic leagues.

 

The hosting was confirmed by CAF president Patrice Motsepe earlier this week on a visit to Kenya. The finals had originally been scheduled for this year.

 

“CHAN is an excellent opportunity for Africa-based players. It is a perfect place to groom tomorrow’s winners of the AFCON,” said Motsepe.

 

“I have no doubt in my mind that Kenya, Uganda and Tanzania will host the best CHAN in the history of the competition because I have seen how willing and committed the governments are.”

 

With three host countries the finals will be expanded to 19 teams. Qualifiers kick off next month.

 

The hosting is a major step forward for the Kenyan FA who were awarded the hosting rights in 2018, but lost them for not being ready to host. The Nyayo and Kasarani Stadia look set to be Kenya’s host stadia with Kenyan president William Ruto guaranteeing that all facilities will be ready.

 

Earlier this year the Kenyan FA came close to suspension from international competition following government interference. Back from the brink, the Kenyans are now hosting major African tournaments.

Post a Comment

0 Comments