Tatizo la vyoo bora Kasulu bado ni kitendawili.

 

(Picha na Kasulu TC).
Wakazi wa mtaa wa mkombozi kata ya Murusi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wameulalamikia uongozi wa mtaa juu ya ukosekanaji wa choo katika mji wa Bi. Eres Toyi ambae ni mkazi wa  eneo hilo.

Akizungumza na Buha news jirani wa mkazi huyo Bi. Ester Ntawiha ameeleza kuwa kukosekanaa kwa choo katika mji huo kunapelekea uchafuzi wa mazingira pia kunahatarisha afya za watoto kutokana na kucheza katika mazingira hayo.

"Sisi kama majirani wake tumempokea mwaka 2021 na alihamia nyumba ikiwa haina choo tukawa tunamsaidia kumruhusu kujisaidia kwenye vyoo vyetu kwa ahadi ya kujenga chake lakini mpaka sasa ni miaka mitatu na hakuna dalili  ya kuchimba shimo la choo hivyo familia yake hujisaidia hovyo katika eneo lake, hali ambayo inahatarisha afya ya watoto wetu kwa maana wanachezea maeneo hayo na mvua ikinyesha inasafirisha kinyesi na kyuchafua mazingira".

Mwenyekiti wa mtaa wa Mkombozi Bw. Fidel Atanas Nkomo amekiri kuwepo kwa kero hiyo na kuelezea hatua walizozichukua kama serikali ya mtaa  nikumpatia muda wa ujenzi wa miundombinu bora ya choo baada ya kukaidi amri  hiyo alipelekwa ngazi za juu.

Nae Mtendaji wa mtaa wa mkombozi Bi. Zipora Biseco amewaasa wananchi wakata hiyo kutokupuuza maagizo wanayopewa na viongozi mbalimbali kuepuka kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Nyumba ya Bi. Eres Toyi anayeishi bila kuwa na choo na kutuhumiwa kuchafua mazingira mjini Kasulu

Akizungumza na Buha News Bi. Eresi Toyi amekiri kuishi katika makazi yake bila kuwa na choo na kueleza kuwa ukosefuu wa pesa ni sababu ya kushindwa kujenga choo na kwamba anaishi maisha duni.

Mkazi wa mtaa wa Mkombozi kata ya Murusi wilaya ya Kasulu Bi. Eres Toyi kulia ni mwanae Evelina Adriano wakiwa katika ofisi za afisa mtendaji wa mtaa kujibuu tuhuma za kutokuwa na choo katika makazii yao

Baada ya kutembelea kaya hiyo Afisa Afya na Usafi wa Mazingira Kasulu Mji Bw. Msafiri Charles ametoa maagizo kwa kaya hiyo kuhakikisha wanakuwa na choo ndani ya siku saba na hatua stahiki dhidi yake zitachukuliwa endapo atakaidi amri hiyo.

Ndugu wa mama huyo ambao wanaishi maeneoo mbalimbalii nchini wamepigiwa simu na kuagizwa kutoa michango ya hali na mali kuwezesha ndugu yaoo kuishi maisha salama katika kaya yenye choo.

Kampeni hii ya Mtu ni Afya imeanzishwa Agosti Mosi 2024 katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu yenye kauli mbiu inayosema 'Fanya kweli usibaki nyuma mtu ni afya'.

MwandishiEllukagha Kyusa.

Mhariri: Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments