Mwanzilishi wa mtandao wa
mawasiliano wa Telegram, Pavel Durov, amesema kuanzia sasa mtandao huo utakuwa
unashirikiana na vyombo vya usalama kuwapa taarifa kuhusiana na uhalifu wa
watumiaji wake.
Durov, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa
mwezi uliopita kwa tuhuma za kushindwa kuchukuwa hatua dhidi ya wahalifu kwenye
mtandao wake, alisema huduma ya kutafuta taarifa ya Telegram imetumika vibaya
na watu wanaouza bidhaa haramu.
Kuanzia sasa, Telegram itakuwa inawapa
maafisa wa usalama taarifa kama vile nambari ya simu na anwani ya mtandaoni ya
wale wanaovunja kanuni za matumizi ya kimtandao.
Durov, mwenye umri wa miaka 39, yuko nje kwa
dhamana, lakini haruhusiwi kusafiri nje ya Ufaransa.
pavel durov alikamatwa mnamo aug 24/8/2024
katika uwanja wa ndege
wa le Bouget Airport huku kukamatwa kwake kukihusishwa na kukataa kushirikiana na vyombo vya usalama juu ya masuala ya ulanguzi wa madawa ya
kulevya, biashara haramu ya binaadamu na udanganyifu wa mtandaoni.
0 Comments