TETESI za soka barani Ulaya.

Wakati mustakabali wa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen,(32), na Mbrazil Casemiro,(32), ukiwa bado mashakani ndani ya Manchester United miamba hiyo ya Old Trafford wanawaza kumnunua kiungo wa kati wa Bayern Munich Mjerumani Leon Goretzka,(29)

Manchester United wanatazamia kumpa kandarasi mpya kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo,(19), ili kuonyesha hadhi yake kama nyota wa kikosi cha kwanza.

Tottenham Hotspur, Chelsea the Blues na Paris St-Germain(PSG) wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania kumsajili mshambuliaji wa Swede Viktor Gyokeres, mwenye miaka 26, kutoka kwa wababe wa Ureno Sporting. 

Aidha Majogoo wa jiji la London Liverpool wanamtazamia beki wa kati wa Juventus na Brazil Gleison Bremer(27), kama mbadala wao bora wa Mholanzi Virgil van Dijk(33).

Newcastle United wanamfuatilia mshambuliaji wa Norway Sindre Walle Egeli(18) huku West Ham, Crystal Palace, Brighton na Brentford pia wakivutiwa na uwezo wa kijana huyo aliyekadiriwa kuwa na thamani ya £25m. 

Beki wa pembeni wa Bayern Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong(23), yuko kwenye orodha ya wachezaji watano walioteuliwa na Chelsea kuchukua nafasi ya beki wa pembeni wa Uingereza Reece James,(24)

    Jeremie Frimpong

Katika hatua nyingine Inter Milan wanataka kumsajili beki wa Arsenal na Japan Takehiro Tomiyasu mwezi Januari huku The Gunners wakihitaji £25m kwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 25.

Manchester City wana wanatazamia kuanza mazungumzo ya kandarasi na kipa Ederson mwenye umri wa miaka 31, huku mkataba wa Mbrazil huyo ukitarajiwa kufika ukingoni  msimu wa joto 2026. 

Ederson Santana

Hata hivyo Fowadi wa Southampton mwenye umri wa miaka 18 Tyler Dibling yuko kwenye rada za Manchester United baada ya kumvutia mkurugenzi wa michezo wa red
 devils Dan Ashworth.

Mwandishi; Eunice Jacob

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments