TETESI za soka Ulaya.

Newcastle wanamfuatilia winga wa Bayern Munich raia wa  Ujerumani Leroy Sane, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kuwa mchezaji huru.

Bayern Munich  wapo kwenye    mazungumzo yakuendelea kupata huduma ya  kiungo wa kati wa kimataifa wa Ujerumani Jamal Musiala, 21, kwa  kuongeza mkataba baada ya mkataba wake  wa sasa ukitarajiwa kutamatika 2026.

AC Milan, Inter Milan na Napoli wote wana nia ya kunasa  Saini ya  kiungo wa kati wa Torino mwenye umri wa miaka 23 Samuele Ricci.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Max Eberl ametetea kuuzwa kwa mlinzi wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 25, kwa Manchester United, akisema mabeki wa kati wa sasa wa klabu hiyo wana uwezo zaidi wa kuweka ulinzi juu zaidi ya uwanja. 

Mwandishi; Eunice Jacob

Post a Comment

0 Comments