THRDC Yazindua mkakati wa kutafuta Rasilimali za ndani.

                                                                                                            (Picha na Ellukagha Kyusa)

Mtandao wa watetezi wa Haki za binadamu Tanzania (THRDC) kwenye mkutano mkuu wa 13 wa mwaka wa wanachama uliofanyika leo Septemba 12,2024 Jijijni Arusha umezindua mkakati maalumu wa ufuatiliaji rasilimali ndani ya nchi ili kuondokana na kasumba ya Azaki kutegemea msaada kutoka mataifa ya nje.

Mwenyekiti wa bodi ya THRDC Pili Mtambalike amesema kuwa Azaki zisizo za kiserikali zinategemea rasilimali kutoka nje ya nchi kwa 90% huku ndani ya nchi wakipata 10% na kuongeza kuwa wahisani toka nje ya nchi wamekuwa wakusuasua hivyo utekelezaji wa kutafuta rasilimali ndani ya nchi ufanyike kwa haraka.

Bw:John Kalage mwenyekiti kamati ya kuandaa mpango wa kutafuta rasilimali THRDC amesema mpango huo utasaidia kuendesha shughuli za haki za kibinadamu nchini Tanzania na kuwasisitiza kuwa ni muda muafaka wa wananchi kubadilika na kuchangia ukuaji wa uchumi na shughuli za kijamii.

Baadhi ya viongozi wa THRDC katika mkutano wa 13 Jijini Arusha  wakikabidhiana nakala ya mkakati. (Picha na Ellukagha Kyusa)

Mgeni rasmi Bw:Raphael Maganga Mkurugenzi wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) amesema mkakati huo unalengo la kuimarisha haki za binadamu kwa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia, mabadiliko ya tabia Nchi ,utawala bora pamoja na kushiriki katika miradi ya kiserikali.

Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) ni mtandao wenye zaidi ya wanachama 200 Tanzania bara na Visiwani ilianza rasmi 2015 nchini ikiwa na lengo la kutetea haki za binadamu na kutoa elimu ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa.

Post a Comment

0 Comments