Tisa wafariki Lebanon.


Watu wasiopungua tisa wamefariki na  Maelfu ya watu wamejeruhiwa nchini Lebanon baada ya vifaa vya mawasiliano "pagers"   kulipuka Beirut.

Hezbollah imesema wapiganaji wake wawili wameuawa katika mkasa huo ulioikumba Lebanon na   wameishutumu Israel kuhusika.. 

Katika hatua nyengine mkuu wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah anatarajiwa kutoa hotuba yake kuhusiana na suala hilo Alhamis ya wiki hii kwa mujibu wa taarifa ya kundi hilo.  

Waziri wa afya  nchini Lebanon Firass Abiad amethibitisha kwamba watu tisa waliuawa kwenye milipuko hiyo akiwemo mtoto mmoja na watu wengine 2,800 wakijeruhiwa ambapo 200 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

 Wizara ya Afya imewatahadharisha watu kutovitumia vifaa hivyo na  kuwaomba  kujitokeza kuchagia damu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imelaani kile ilichokilezea kama "kitendo cha makusudi na cha hatari kinachofanywa na Israel cha kuusambaza mzozo na mpaka sasa Israel bado haijasema chochote juu ya mkasa huo.

Mashuhuda wamesema mji wa Beirut umekumbwa na hamaki kubwa na kumeshuhudiwa magari mengi ya wagonjwa baada ya milipuko hiyo.

Tangu kuanza kwa makabiliano makali Oktoba, 2023 kati ya wanajeshi wa Israel na Hamas ambao ni washirika wa karibu na kundi la Hezbollah  nchini Lebanon yamesababisha vifo vya mamia ya wapiganaji wengi nchini Lebanon na kadhaa wakiwemo wanajeshi wa upande wa Israel.

 

Mwandishi:Abel  mahenge.

Mhariri: Ellukagha Kyusa.


Post a Comment

0 Comments