Waziri mkuu ameyasema hayo Septemba 6,2024 wakati akitoa hotuba ya akuhahirisha mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania Jijini Dodoma, na kusisitiza wananchi kutunza chakula ili kuepukana na janga la njaa linaloweza kusababishwa na mabadiliko ya Tabianchi kama ilivyoelekezwa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania(TMA).
"Nitowe rai kwa wananchi kutumia vizuri mavuno yaliyopatikana msimu wa 2023/2024 kwa kutunza chakula cha kutosha katika ngazi ya kaya na kuzigatia kanuani bora za uhifadhi wa mazao ya chakula" Ameseama Majaliwa.
Akiendelea kutoa rai hiyo Majaliwa amesema baadhi ya mikoa , wananchi wantakiwa kuchukua tahadhari mapema na kuzalisha mazao yanayokomaa kwa muda mfupi zaidi ili kuepuka upungufu wachakula.
"Nachukua nafasi hii kuwahimiza wananchi kupanda aina ya mazao yanayokoma kwa muda mfupi na kustahimili ukame ili kuepuka upungufu wa chakula "
Aidha Mh. Majaliwa amewataka Maofisa Ugani kuhakikisha wanawaelimisha wananchi kuhusu mazao yanayopaswa kupandwa maeneo yao.
Moja ya Ghala la hifadhi ya chakula nchini. (Picha na wizara ya Kilimo)
Akizungumza kuhusu uhifadhi wa chakula nchini ameseama serikali kupitia wakala wa uhifadhi wa chakula inaendelea kununua ziada ya mazao ya chakula yaliyopatikana kutoka kwa wakulima kwa ajili ya akiba ya chakula na sehemu ya hifadhi hiyo itatumika kusadia maeneo yatakayobainika kuwa na upungfu wa chakula.
Wakati huo huo Majaliwa ameagiza wizara ya kilimo isimamie kwa karibu upatikanaji wa pembejeo za kilimo hususani mbolea ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao wa kilimo kwa kuzingatia Jiografia za kanda za kilimo nchini.
Mkutano wa 16 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania umeputisha Miswada nane ukiwemo mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria za hifadhi ya jamii ya mwaka 2024, mkutano huo umehairishwa hadi Octoba 29,2024.
Mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA) ilitoa tahadhari ya upungufu wa mvua za vuli katika mikoa mbalimbali nchini, Agosti 22, 2024 wakati wakitoa mwelekeo wa msimu wa mvua vuli kuanzia Octoba mpaka Disemba mwaka huu
Mwandishi; Harieth Kamugisha
0 Comments