Trump hatarini baada ya shambulizi la mara ya pili.

Rais wa zamani wa na mgombea uraisi wa Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump ameshambuliwa mara ya pili kwa risasi mjini Florida Marekani.

Shambulizi hilo limetokea siku ya Jumapili mjini Florida karibu na uwanja wake wa mpira wa Gofu uliopo West Palm Beach huku mgombea huyo akisema kuwa yuko salama juu ya shambulizi hilo.

Kwa upande wa shirika la ujasusi nchini humo FBI limesema kuwa wanaendelea kuchunguza kwa karibu tukio hilo huku wakidhibitisha kukamatwa kwa mshukiwa wa tukio hilo.

Kwa upande wake makamu wa Rais wa Marekani na mpinzani mkuu wa Trump katika uchaguzi wa mwaka 2024, Kamala Harris kupitia ikulu ya White House amesema kuwa amesikitshwa na jaribio la mauaji wa Rais wa zamani wa taifa hilo.

Awali gazeti la Washington Post nchini humo limetoa taarifa kuwa Trump alikuwa akicheza Gofu kwenye uwanja huo wakati lilipotokea tukio hilo na maafisa wa Idara ya Ulinzi wa Viongozi walimkimbiza kwenye chumba maalumu cha maficho kilichopo kwenye uwanja huo.

Tukio hilo linakuja miezi miwili tangu Julai 13,2024 tangu Trump kushambuliwa na mtu mwenye silaha katika mkutano wa hadhara uliofanyika Butler, Pennsylvania na kujeruhiwa upande wa pili wa sikio.

Mwandishi; Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments