Maelfu kuandikishwa mkoa ya Mara, Simiyu na Manyara

 

 




Mikoa ya Mara,Simiyu  na baadhi ya halmashauri za mkoa wa Manyara inatarajiwa  kuanza zoezi la uboreshaji wa daftarai la kudumu lawapiga kura  kwa muda wa siku saba kuanzia tarehe o4  hadi 10 septemba ,2024 ,ambapo jumla ya wapiga kura wapya 491,050 wanatarajiwa kuandikishwa.


Hata hivyo,  Mkurugenzi  wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan  asesema idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi.

 

Idadi hii inaweza kuongezeka kwa kuwa inawezekana wapo watanzania ambao walikuwa na sifa za kuandikishwa kuwa wapiga kura wakati wa uboreshaji wa Daftari mwaka 2019/20, lakini kwa sababu moja au nyingine hawakuweza kujiandikisha kuwa wapiga kura,” amesema Bw. Kailima.

 

 Jumla ya vituo 4,373 vinatarajiwa kutumika kuwaandikisha wapiga kura wapya na kuboresha taarifa za wapiga kura walioandikishwa kwa awamu zilizopita huku vituo vya uandikishaji vikitarajiwa  kufunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni  .

 

Uboreshaji wa Daftari  la kudumu la wapiga kura kwenye mikoa hiyo unafanyika ikiwa ni mwendelezo wa zoezi hilo lililozinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2024 ,Ukijumlisha   mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora Ukifuatiwa na Mikoa Kagera na Geita pamoja na  mikoa ya Mwanza na Shinyanga .

 

 Kwa mujibu wa makadirio yaliyofanywa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC) kutokana na  takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, idadi ya wapiga kura 3,391,017 wanatarajiwa kuwemo kwenye Daftari la Kudumumu la Wapiga Kura kwenye mikoa hiyo wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.


Maboresho ya daftari la kudumu la wapiga kura hufanyika kila baaada ya miaka minne ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu na tayari  tume huru  ya taifa ya uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika Novemba 27 ,2024 .

 

Mwandishi :Mroki Mroki 

Post a Comment

0 Comments