Ujenzi wa barabara ya mwendokasi Segerea upo pale pale

Mpango wa Serikali kujenga Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi jimboni Segerea, haujabatilishwa licha ya jamii kuwa na hofu na wanaotakiwa kupisha Mradi huo wamehakikishiwa kulipwa fidia zaoo kwa wakati. 

Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi John Mkumbo, amethibitisha hayoo mapema leo wakatii wa mahojiano maalumu na mwandishi wa Buha News aliyefika TANROADS kutaka kujua kuhusu mikakatii ya utekelezaji wa mpango huo

Mhandisi Mkumbo ameomba wananchi waendelee kuvumilia wakati Serikali ikikamilisha taratibu za kuwalipa fidia, ili wapishe mradi kwa mujibu wa Sheria.

Mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati ya kitaifa, ambayo inatekelezwa chini ya Mamlaka ya Barabara Tanzania (TANROADS). 

“Tunafahamu wajibu wetu kwao, Bunge Liliuokalani pitisha Jedwali la fedha za huu mradi, tukaandika maombi kwa wizara ili tupatiwe hizo fedha, tunasubiria,” amesema Mhandisi Mkumbo. 

Akijibu ikiwa uthamini utarudiwa kufuatia muda mrefu kupita tangu uthamini wa mwisho ulipofanywa Mwaka 2022, Mhandisi Mkumbo amesema; “Ninachofahamu Mimi shughuli hizi zinafanywa kwa mujibu wa sheria, kuna vipengele vinavyoelekeza cha kufanya katika mazingira ya namna hii.”

Baadhi ya wakazi jimboni Segerea, wanaishi  kwenye makazi yaliyowekewa alama ya X tangu Mwaka 2019,  ulipofanyika uthamini kwa mara ya kwanza, kabla haujarudiea Mwaka 2022.

Kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi pamoja na malipo baada ya taathimini kutofanyika kwa wakati kumekuwa kukisababisha malalamiko na sintofahamu kuhusu nini kitalipwa wakati uthamini ulifanyika miaka kadhaa iliyopita huku thamani ya pesa na mali ikibadilika

Daniel Ngowi, ambaye ni mmoja wa wakazi wa Tabata Aroma amesema wakati utamini huo wa Pili ukifanywa, waliahidiwa kuwalipa fidia ndani ya kipindi kisichozidi Miezi Sita, ahadi ambayo mpaka sasa haijatekelezwa.

“Majuzi Mbunge wetu (Bonah Kamoli) alitueleza kwenye mkutano wa hadhara kwamba tuendelee na maisha Kama kawaida, serikali ikiwa tayari watakuja tufanye mazungumzo upya,” amesema Ngowi.

Mpango wa Ujenzi wa barabara kwa ajili ya mradi wa mabasi ya mwendokasi katika Jimbo la segerea ni miongoni mwa mikakati ya serikali ya kuboresha miundombinu ya usafiri jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi unaendelea katika mmaeneo mengine ikiwemo Mwenge na Mbagara.

Mwandishi: Editha Majura, Dar Es Salaam.

Post a Comment

0 Comments