Ujerumani kutoa msaada wa kibinadamu Gaza.

                                                                                                                              Picha:DW
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Berlin itaongeza misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kwa kiasi cha Euro bilioni 50.

Baerbock ametoa tangazo hilo katika mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman al-Safadi mjini Amman akinukuliwa na DW akiongeza kuwa kiasi kilichotolewa na Ujerumani kwa Ukanda wa Gaza tangu mwaka jana ni zaidi ya Euro milioni 360.misaada hiyo itaelekezwa kupambana na njaa, utapiamlo pamoja na utoaji wa huduma za afya.

Ujerumani pia itaongeza msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan kwa kiasi cha euro milioni 12.7, na kuongeza msaada kwa Jordan hadi Euro milioni 63.

Kabla ya safari yake nchini Jordan, Baerbock alitembelea Saudi Arabia na anatarajiwa kuzuru Israel katika  ziara yake ya Mashariki ya Kati.

Mwandishi; Ellukagha Kyusa

Post a Comment

0 Comments