Matukio ya ukatili kizungu mkuti mkoa wa kigoma.

                                                             Picha na Sharifat shinji Buha News.

Mkoa wa Kigoma umetajwa kuwa miongoni mwa mikoa  yenye kiwango kikubwa cha ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto nchini Tanzania.

Akitoa Takwimu ya maendeleo ya dawati mbele ya maofisa  kutoka ukanda wa (NORDIC) inayojumuisha nchi tatu ambazo ni Norwa,Sweden na Canada, mkuu wa dawati la jinsia na watoto la Polisi mkoa wa kigoma Inspekta  Michael  Mjema amebainisha kuwa matukio ya ukatili yamezidi kuongezeka kutoka kesi 835 kwa mwaka 2022 hadi kesi 1647 kwa mwaka 2023 ikiwa ni ongezeko la kesi 812 kwa mwaka mmoja.   

"Kulingana na takwimu hizi kumekuwa na ongezeko la kesi za ukatili wa kijinsia kwa mwaka mzima kama zinavyoonekana hapa kuanzia mwaka 2017 hadi 2023 kumekuwa na ongezeko kubwa  mfano 2022 kesi za ukatili kwa mkoa mzima zilikuwa 835 pekee lakini kila kukicha yanaongezeka  ingawa kutokana na elimu tunayoitowa kwenye jamii wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa wa kuripoti matukio hayo" 

Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa wa kigoma Inspector Michael  Mjema  akitoa maelezo kuhusu   hali  ya ukatili wa kijinsia Wilayani. Picha na Sharifat shinji Buha News

Kwa upande wake msimamizi wa dawati la jinsia wilaya ya kasulu mkaguzi Maimuna Abdul amewashukuru wadau wa kimataifa kuendelea kushirikiana katika kutokomeza matukio ya ukatili katika wilaya ya Kasulu na mkoa mzima wa kigoma.

"Umoja wa Mataifa UN umekuwa ni mchango mkubwa kwa wilaya ya Kasulu kwani wameendelea kushirikiana na sisi toka mwanzo na wamefanikisha kukamilisha jengo kubwa hili hivyo ni jambo la kujivunia katika wilaya yetu ya Kasulu".

    Picha na Sharifat Shinji Buha News
Kwa upande wa wageni  kutoka ukanda wa (NORDIC)  wamepongeza Dawati la jinsia na watoto la Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kwa hatua ya kutoa elimu ya ukatili kwenye jamii ambayo imesaidia wananchi kuripoti vitendo vya ukatili mkoani humo.

Wageni hao kutoka ukanda wa Norway,Sweden na Canada  (NORDIC) walitembelea dawati la jinsia na watoto la Polisi mkoani Kigoma kwa lengo la kujionea namna jeshi hilo la polisi linavyoshughulikia matukio ya ulatili wa kijisia.

Mwandishi; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments