Vision care yaipa Muhimbili mashine mbili za upasuaji wa macho

 


Hosipitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea mashine mbili za kisasa zinazogharimu Tsh. 68,247,700 kwa ajili ya upasuaji wa macho kwa njia ya tundu dogo kwa wagonjwa wenye tatizo la mtoto wa jicho. 

Vifaa hivyo (surgical consumable and medicine na phacoimuisifier) vimetolewa na Vision Care kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA).

Bingwa wa Macho na Mkuu wa Idara ya Macho MNH, Dk. Joachim Kilemile, akizungumza septemba 18 jijini Dar es Salaam kuhusu kambi ya mafunzo ya siku tano ya kupokea mashine hizo, amesema vifaa hivyo vitarahisisha matibabu, kuokoa  muda  wagonjwa  na kupona mapema.

" mashine hii imeongeza ubora kwa sababu awali kwa mgonjwa mwenye mtoto wa jicho alitakiwa asubiri upasuaji hadi mtoto wa jicho akomae ila kwa sasa upasuaji hautasubiri hilo atafanyiwa mara tu atakapobainika, kwa gharama nafuu"alisema Dk. Kilemile.

Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Vision Care duniani, Dk. Dong Hae Kim, amesema taasisi hiyo imeamua kushirikiana na MNH kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu pamoja na kutoa vifaa na kuongeza kuwa mafunzo hayo ni pamoja na namna ya kutumia mashine hizo kwa matokeo bora ya matibabu, kwa kuwa vifaa hivyo vimekwishatumiwa  miongoni mwa madaktari bingwa wa macho.

Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji MNH, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji MNH, Dk. Ibrahim Nkoma, amesema upasuaji wa tundu dogo utafanyika kwa asilimia 60 hadi 70 na kwamba kati ya wagonjwa 10 wanaohudumiwa miongoni mwao sita watapatiwa huduma hiyo, na  MNH itawatumia wataalamu wake waliojengewa uwezo kuwapa mafunzo wenzao katika hospitali za kanda, rufaa, mikoa na wilaya ili  kuwapatia huduma wagonjwa huko waliko.

 

Mwandishi ;Ellukagha kyusa

Mhariri Abel Mahenge

Post a Comment

0 Comments