Vita ya Hezbollah na Israel yazalisha wakimbizi zaidi ya 80,000 wa Lebanon


Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa  kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amesema takribani wakimbizi Elfu themanini (80,000) wamekimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Lebanon. 

Amesema hayo septemba 30,2024  kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaedelea kutoa msaada katika vivuko vinne vya mpakani huku takriban watu 80,000 wakikimbilia Nchini Syria katika muda wa siku saba zilizopita  na kati ya hao, 36,000 walikuwa Wasiria na 41,300 walikuwa Walebanon.

Wakati huohuo Shirika la habari la BBC limeripoti wasiwasi walionao Waafrika waishio nchini Lebanon kutokana na kile  kinachoendelea nchini humo na kudai kuwa wanajiandaa kuondoka kurudi Afrika kusubiri Mgogoro huo ukamilike 

Awali kundi la wapiganaji la Kipalestina Hamas, limesema kuwa kiongozi wake nchini Lebanon Fateh Sherif Abu el-Amin ameuawa pamoja na baadhi ya washirika wake katika shambulio la anga la Israel kusini mwa Lebanon.

Jeshi la ulinzi la Israel (IDF) kupitia kwa waziri mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu limekiri kuhusika katika mashambulizi na kushambulia kwa mabomu maeneo mengine kusini mwa Lebanon yanayotumiwa na Hezbollah kutekeleza operesheni za kiaidi dhidi ya Israel.

Israel imeendelea kuishambulia Lebanon takribani wiki moja tangu kuanza kwa mashambulizi hayo huku wizara ya afya nchini lebanion ikiripoti kuuawa kwa wananchini wake wasiopungua 700 kutokana na mashambulizi Israel nchini humo.

Mwandishi: Ramadhan Zaidy 

Mhariri : Harieth Kamugisha 

Post a Comment

0 Comments