Mh.Bashungwa amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma katika kikao cha 16 mkutano wa 5 wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Dkt Florence Samizi aliyetaka kujua ni lini serikali italipa fidia ya wananchi wa Muhambwe waliopisha ujenzi wa barabara ya Kibondo hadi Mabamba mkoani humo .
Aidha waziri Bashungwa ameongeza kuwa serikali imekamilisha tathimini ya mali za wananchi zitakazoathiriwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo hadi Mabamba yenye urefu wa kilometa 47.92 huku kusisitiza kuwa serikali inakamilisha taratibu zote za malipo ya fidia kwa wananchi hao .
Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo ulitiwa saini tarehe 8 Januari 2023 kati ya serikali na kampuni ya ujenzi kutoka China (CHICO) huku kazi ya ujenzi wa barabara hiyo ukitarajiwa kufanyika ndani ya miezi 24 na mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 63.
Na mwandishi :Ramadhani Zaidy
0 Comments