Wafanyabiashara wa samaki katika soko la Mnadani,Kata ya Kigondo ,Halmashauri ya mji
wa Kasulu , wameeleza kuridhishwa na bie ya samaki kuendelea kupungua baada ya ziwa
Tanganyika kufunguliwa mwezi mmoja uliopita .
Wakizungumza na Buha News bila kutaja majina yao wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa bei ya ndoo moja ya samaki aina ya Migebuka ni shilingi 135,000 Kutoka 165,000 iliyokuwepo
wiki moja iliyopita.
“Kwasasasa bei imeshuka tunashukuru sana wiki moja
iliyopita tulikuwa tunanunua 165,000/= ndoo lakini wanaendelea kushuka bei hadi imefikia kiasi cha shilingi 135,000/= “Alisema mmoja wa wafanyabiashara hao
Aidha Wamesema fungu moja lenye samaki saba hadi nane linauzwa shilingi 2000/= kwasasa ambapo awali walikuwa wanauza fungu lenye samaki wanne kwa bei hiyo huku akibainisha kuwa ongezeko la wateja limewafanya kuongeza kipato na kukuza uchumikatika familia zao na nchi kwa ujumla.
Ziwa Tanganyika lilifunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 15 mei mpaka tarehe 16 agosti mwaka 2024 ,na baada ya kufunguli kwa ziwa hilo wavuvi na walanguzi wa samaki wanakiri kuona matokeo chanya ya kufungwa kwa ziwa hilo.
Mwaka 2023 kulikuwa na ukosefu wa dagaa na samaki kabla ya ziwa kufungwa, huku upatikanaji wa samaki na dagaa ukiripotiwa kupande bei kufikia elfu 55 hadi elfu 60 kwa kilo moja kutoka elfu 10 ya mwanzo.
Hata hivyo waziri mwenye dhamana Abdallah Ulega wakati
akizungumza na wananchi alisema kufungwa
kwa ziwa hilo ni makubaliano yaliyoazimiwa katika kikao kilichofanyika mwaka
2022, kilichohusisha nchi zinazo zunguka ziwa hilo ambazo ni Zambia,Tanzania
,Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC).
Ifahamika kuwa tarehe 15 mwezi mei mwaka 2024 Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma lilifungwa ili kupisha mazaliya ya samaki pamoja na kukomesha uvuvi haramu,jambo liloleta taharuki kwa wavuvi wa mikoa inayozunguka ziwa hilo ikiwemo mkoa wa Kigoma ,Katavi na Rukwa.
Mwandishi; Harieth Dominick.
Mhariri; Eunice Jacob.
0 Comments