Wananchi wilayani Kibondo mkoani Kigoma wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika kote Nchini mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu,ili kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Msimamizi mkuu wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
Deoclets Rutema wakati wa mkutano wa kuhamasisha upigaji kura na kutoa elimu
uliofanyika katika Kijiji cha Kigina kata ya Rugongwe.
Bw. Rutema amesema ili kuwapata viongozi bora, katika uchaguzi huo wananchi
wanapaswa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi pamoja na kushiriki
kikamilifu kupiga kura kuchagua viongozi sahihi watakao leta mabadiliko ya maendeleo
katika maeneo husika.

kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura havihusiki na uchaguzi wa serikali zaMitaa hivyo wajitokeze kujiandikisha katika daftari la uchaguzi wa serikali za mitaautakaonza hivi karibuni .
Bw. Ndarangavye amongeza kuwa kupata viongozi bora wananchi waepuke kuchagua
wagombea wanaotoa rushwa ambao hutaka madarada ili kujinufaisha kwa faida yao.
Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu,,huku
uandikishaji wa wapiga kura wa serikali za mitaa ukianza tarehe 11
hadi 20 mwezi Octoba 2024 katika mitaa husika na kampeni za uchaguzi wa serikali za
mitaa zitaanzaNovemba 20 hadi 26 mwaka huu .
Mwandishi : James Jovin
Mhariri : Harieth Kamugisha
0 Comments