Waliofariki kwa ajali ya moto Nigeria wafikia 59.

                          Reuters

Idadi ya watu walio fariki kwa ajali ya moto wa lori la mafuta Nigeria imefikia 59 kutoka 52 walio tajwa mapema leo septemba 9.

Ajali hiyo iliyo sababishwa na lori la mafuta kugongana na lori lingine lililokuwa limebeba wasafiri na ng'ombe 50 ilitokea jana jumapili septemba 8,2024 kaskazini mwa Nigeria

Wakati huo huo shirika la Habari DW limeripoti kuwa idadi hiyo ya watu waliofariki tayari  wamezikwa.

 Kwa upande wake Gavana wa jimbo hilo Mohammed Bago aliwataka madereva kuchukua tahadhari na kuzingatia kanuni za usalama barabarani ili kuzuia majanga hayo.

Ajali mbaya za barabarani zinazohusisha magari ya mafuta hutokea mara kwa mara nchini Nigeria, huku ajali 1,531 zikirekodiwa mwaka 2020 pekee,BBC na kusababisha vifo vya watu 535 na wengine 1,142 kujeruhiwa, kulingana na Kikosi cha Kitaifa cha Usalama Barabarani.

Mwandishi; Ramadhan Zaidy.



Post a Comment

0 Comments