Wanafunzi wa darasa la saba wakifanya mtihani .
Zaidi ya wanafunzi milioni moja na laki mbili wameanza mtihani wao wa kuhitimu elimu ya msingi unaonza leo septemba 11 hadi septemba 12 ,2024 .
Kwa mujibu wa Baraza la mithani Tanzania NECTA watahiniwa wa jinsia ya kike ni laki 6 elfu sitini na sita mia sita na nne (666,604) ambayo ni sawa na asilimia 54 wakati wavulana ni laki tano elfu sitini na nne mia moja sabini sita (564,176) sawa na asilimia 46 ya wavulana wote .
Hata hivyo katika taarifa iliyotolewa na baraza la mitihani Tanzania septemba 10, 2024 imesema wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaofanya mtihani wa darasa la saba 2024 ni 4583 .
"Wanafunzi wasioona ni 98 ,wenye uono afifu 1402 ,wenye uziwi ni wanafunzi 1067 ,wanafunzi 486 wana ulemavu wa akili pamoja na wanafunzi 1530 wenye ulemavu wa viungo " Alisema katibu wa baraza la Mitihani Tanzania Dkt Mohamed
wakati watahiniwa wa mwaka 2024 wakiwa 1230780 kuna upungufu wa watahini 125,612 ikilinganishwa na watahiniwa 1,397,293 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2023.
Lengo la mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi nikupima maarifa na umahiri waliopata wanafunzi kwa miaka saba na matokeo yake hutumika kuchagua wanafunzi watakao jiunga na elimu ya sekondari.
Mwandishi; Ramadhani Zaidy
0 Comments