Tetesi za Soka la Ulaya septemba 21,2024



Barcelona, Atletico Madrid na Bayern Munich ni miongoni mwa vilabu vinavyomhitaji
 mshambuliaji wa Marseille Mwingereza Mason Greenwood mwenye miaka 22. 

PSG wanamtaka mshambuliaji wa Newcastle raia wa Uswidi Alexander Isak huku Magpies ikiweka thamani ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuwa takriban euro 100m (£83.8m).

Chelsea wanataka kumuuza mlinzi wa kimataifa wa  Ufaransa Axel Disasi mwenye umri wa miaka 26 katika dirisha la uhamisho la Januari.

Nottingham Forest inawafuatilia wachezaji wawili wa kimataifa wa Uturuki, winga wa Galatasaray Baris Alper Yilmaz, 24, na mshambuliaji wa Besiktas Semih Kilicsoy, 19.

Juventus watatafuta kumsajili mshambuliaji wa Lille nchini  Canada Jonathan David mwenye umri wa miaka 24 mnamo mwezi Januari kwa mkataba wa euro 15m (£12.5m).

Real Madrid inafikiria kufikia kiwango cha euro 45m (£37.7m), ambacho ni kipengele cha lazima katika suala la kumuuza beki wa Valencia mwenye umri wa miaka 19 kutoka Uhispania Yarek Gasiorowski. 
Everton itampa mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin fursa ya mwisho ya kusaini mkataba mpya kabla ya mkataba wake kumalizika msimu ujao wa joto, huku Newcastle wakionyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. 

Mazungumzo ya mkataba wa mlinzi wa England yamegonga mwamba kati ya Southampton na  Kyle Walker-Peters, mwenye miaka 27 , huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo   ukikamilika msimu ujao wa joto. 

Mwandishi:Eunice Jacob 

Mhariri: Harieth Dominick    

Post a Comment

0 Comments