Picha na BBC
Mkurugenzi
wa oparesheni ya mamlaka ya ulinzi na usalama wa Hamas, amesema kuwa
takriban watu 40 wameuawa kusini mwa Gaza na wengine 60 kujeruhiwa katika
shambulizi lililofanywa na Israel kwenye aneo lililochaguliwa kuwa la
kibinaadamu.
Kwa
mujibu wa shirika la utangazaji la BBC Mkurugenzi huyo amesema shambulio hilo
limetokea usiku wa kumakia September 10,2024 katika eneo la kibinaadamu la
Al-Mawasi magharibi mwa jiji la khan younis.
Kwa upande wa jeshi la Israel kupitia kwa msemaji wa jeshi hilo (IDF) limekiri kuhusika na shambulizi hilo na kusema kuwa ndege yake ilishambulia katika meneo ya khan younis eneo la wapiganaji wa Hamas na kudai kuwa ilichukua hatua za kiusalama ili kupunguza hatari ya kudhuru raia.
wakazi wa eneo hilo pamopja na mashuhuda wa mlipuko uliotokea wanasema mlipuko ulitikisa maeneo ya al-Mawasi muda mfupi baada ya saa sita usiku ,na miali ya moto ilionekana kupanda angani usiku wa shambulizi hilo.
Huu
ni muendelezo wa mashambulizi ya jeshi
la Israel (IDF) dhidi ya kikosi cha Hamas kwani katika juma lililopita wizara ya afya ya
Palestina ilitoa taarifa juu ya kuuawa
kwa wapalestina takribani 36 kutoka katika miji ya Jenin na Tubas huku wengi
wao wakiwa ni watoto.
Mgogoro huu wa Israel na Hamas ukanda wa Gaza ulianza octoba 7,2023 baada ya kundi la wanamgambo wa Hamas kuishambulia Isreal kwa makombora .
Mwandishi: Shukuruimana Revokatus.
0 Comments