Wapalestina 11 wafariki dunia katika Ukanda wa Gaza


Watu 11 wamefariki dunia katika ukanda wa Gaza kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya Israel na HAMAS.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha aljazeera vifo hivyo vimetokea karibu na eneo  Dier al Balah mjini Gaza ikitajwa   kuwa vifo hivyo vimetokana na makombora yaliyorushwa na majeshi ya Israel.

Wakati huo huo shirika la habari la Reuters limeripoti Maandamano ya wananchi yakiongozwa na chama cha wafanya kazi yanayondelea nchini Israel kumshinikiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bw. Benjamin Netanyahu kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas, maandamao hayo yanakuja baada ya vifo vya mateka sita wa Israel.

Umati wa watu unaokadiriwa kufikia 500,000 waliandamana mjini Jerusalem, Tel Aviv na miji mingine, wakimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kuwarejesha nyumbani mateka 101 waliosalia, ikikadiliwa kuwa  theluthi moja ya mateka hao ni Maafisa wa Israel.

Hata hivyo hali ya wasiwasi inaongezeka  kutokana na  uongozi wa nchi hiyo kushindwa kupata makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yangewaachia huru mateka wa Israel.

Ifahamike kuwa vita kati ya Israel na Hamas vilianza  October 7 mwaka 2023 baada ya Hamas kuishambulia Israel kwa makombola ya kushitukiza.

Imeandikwa: Harieth Kamugisha na Sharifat Shinji


Post a Comment

0 Comments