DW
Watoto takribani milioni 2.8 ,Afrika Magharibi na Afrika ya kati wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na mizozo
ya kisiasa katika baadhi ya mataifa katika ukanda huo.
Kutokana na Takwimu
zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha zaidi ya shule 14,000 kutoka nchi
24 zilizopo ukanda wa Sahara na Kongo zililazimika kufungwa katika robo ya pili
mwaka huu.
Takwimu hizo za Umoja wa Mataifa
zimebainisha kuwa, shule 1,457 zililazimika kufungwa tangu
mwanzoni mwa mwaka mwaka huu , ikiwa Jumla ya watoto milioni 57 wenye umri kati ya
miaka mitano hadi kumi na minne kutoka Magharibi na Afrika ya kati hawahudhurii
masomo kutokana na mizozo inayoendelea.
Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kulinda elimu, Baraza la wakimbizi la Norway (NRC) lilisema mataifa yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na Burkina Faso, Mali, Cameroon na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na mizozo ya kivita inayoendelea .
Mwandishi; Sharifat Shinji
0 Comments