WHO yatoa wito kwa Dunia kuhusu Sudan.

Mkurugenzi  mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amelani vikali kwa kitendo cha Umoja wa Mataifa kutojali mzozo unaoendelea nchini Sudan alipokua kwenye ziara katika mji wa Port Said ambayo ni  makao makuu ya muda ya serikali.

Kauli hiyo ameitoa leo Septemba 8, 2024 wakati akizungumza na wandishi wa habari na kudai  kwamba kiwango cha mzozo ni cha kushtusha na kwamba hatua za kudhibiti ugomvi na kupunguza maafa miongoni mwa raia wa nchi hiyo.

"Kulingana na takwimu zilizopo, ugomvi wa Sudan hadi hivi sasa umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 20, kumbuka hiyo ikiwa ni idadi ya chini, kuna watu milioni 10 wamelazimika kukimbia makazi yao na kubaki ndani ya nchi, huku milioni 2 wamelazimika kukimbilia nchi za jirani" 

Aidha Tedros ametoa wito wa kusitishwa mara moja vita na kufikia makubaliano yatakayopelekea suluhisho la kudumu la kisiasa na anatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuamka na kuisaidia Sudan. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani,(WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus (katikati) na kushoto kwake ni mwakilishi wa Mashariki ya Kati wa WHO,Hanan Balkhv katika hospitali ya watoto mjini Port Sudan.  (Picha AFP)

Katika hatua nyingine Mkuu huyo aliwatembelea wagonjwa katika hospitali moja huko Port Said na kukutana na maafisa wa serikali alipokua ananza ziara ya siku mbili katika mji huo unaoshikiliwa na serikali baada ya kufukuzwa Khartoum na kikosi cha dharura cha Sudan RSF.

Kwa mujibu VOA, Kulingana na mashahidi walozungumza na shirika la habari la AFP, mamia ya watu walikimbilia vitongoji vya kaskazini mwa Khartoum Jumamosi kufuatia mapigano makali kati ya jeshi na kikosi cha dharura karibu na kambi muhimu ya kijeshi.

Watu walokimbia vita na kukwama katika wilaya ya Tokar katika jimbo la Sham kufatia mafuriko makubwa mashariki ya Sudan. (Picha AFP)

Kulingana na Taarifa kutoka rfi kuwa, wataalamu wanatoa wito wa kuundwa kwa utaratibu maalumu wa mahakama kwa ajili ya Sudan, sambamba na hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai.

Mwandishi; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments