WIZARA: Nyumba kwa nyumba kufanya vipimo vya afya.

Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais -Tamisemi imekusudia kutoa mafunzo rasmi ya kuwajengea uwezo watoa huduma za Afya ngazi ya jamii 11,515 kuanzia Septemba 30, 2024  ili kufanikisha azma ya Mpango Jumuishi wa wahudumu hao na kuendeleza afua jumuishi za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii. 

Akizungumza Septemba 19, 2024 Waziri wa Afya Mhe.Jenista Mhagama  katika ofisi ndogo  za wizara hiyo (NIMR) Jijini Dar es Salaam na amesema wizara ina mpango wakuanzisha mafunzo kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii kwa mikoa 11 ya Tanzania Bara.
"Mikoa ambayo itafikiwa na huduma hii kwa Awamu ya kwanza ni pamoja na Geita, Pwani, Tanga, Songwe, Mbeya, Lindi, Tabora, Kagera, Njombe, Ruvuma, na Kigoma" ameainisha waziri Mhagama na kuongeza kuwa"Amesema  Mhagama.

Katika ripoti yake Waziri Mhagama ameendelea kwa kusema kuwa jumla ya wanajamii 31,275 walijitokeza kuomba nafasi huku wanajamii elfu 21,574 waliokidhi vigezo kwenye hatua ya awali walichaguliwa.

“Kwa awamu ya kwanza zoezi la kuwachagua wahudumu wa afya Ngazi ya Jamii lilifanyika kati ya Juni, 8,2024 hadi Julai 25,2024 kwenye Halmashauri 21 kwa mikoa kumi na kuleta idadi ya waliokidhi vigezo elfu 21,574 katika mikoa 11 tuliyoorodhesha hapo awali.

Aidha amesema kuwa wahudumu hao baada ya kupata mafunzo  watapewa vifaa vya kupima malaria kwa haraka na mgonjwa kupewa dawa za awali za ugonjwa huo na kuelekezwa kwenda kupata matibabu zaidi katika kituo cha afya.

"Baada ya mafunzo haya wahudumu tutawapa vifaa vya kupima malaria haraka ili waweze kutoa dawa za awal;i za ugonjwa wa malaria pia watawaelekeza wagojwa kwenda katika vituo vya Afya kwa ajiri ya matibabu zaidi" Imeripotiwa na habari leo

Katika hatua nyingine Amebainisha kuwa majibu yatakuwa siri ya mtu lakini mwanajamii atashauriwa kwenda vituo vya afya na pia wahudumu watapewa Vishkwambi kwaajili ya kuhifazi taarifa.

"Na kuna kipimo cha udumavu watoto watapimwa kwenye mkono kama wanaudumavu itaonesha ni kipimo rahisi,tutawapa mavazi maalum na viatu ,koti la mvua na tumeweka utaratibu wa vifaa vingine muhimu"

Mpango huu ulihusisha jumla ya mitaa elfu 1044, vijiji 754, na vitongoji elfu 3,853 baada ya uchaguzi kupitia mikutano ya jamii jumla ya wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii elfu 9,492 walichaguliwa.

Mwandishi; Abel Mahenge

Mhariri; Sharifat Shinji

Post a Comment

0 Comments