Zelensky anatazamiwa kukutana na Kansela Olaf Scholz.

                                                                                                     Picha:Ukrainian Presidential Press/AFP
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa  kukutana hii leo na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz mjini Frankfurt, kulingana na msemaji wa serikali ya Berlin.

Mazungumzo ya ana kwa ana ya viongoz hao, yatafanyika wakati washirika wa kijeshi wa Ukraine ikiwemo Marekani, wakikusanyika katika kambi ya anga ya Washington iliyoko Ujerumani kuratibu uungaji mkono zaidi kwa Kyiv.

Gazeti la Ujerumani la Der Spiegel limeripoti kwamba Zelensky pia atahudhuria mkutano huo katika kituo cha anga cha Ramstein, kusini magharibi mwa Frankfurt Iikinukuliwa na DW.

Zelensky atajaribu kuwarai washirika wake msaada zaidi kwa mujibu wa gazeti hilo, ikiwa ni siku chache baada ya watu 55 kuuawa na 300 kujeruhiwa katika shambulio la kombora la Urusi kwenye mji wa Poltava.

Mwandishi;Abel Mahenge

Post a Comment

0 Comments