"Ahmed Ally" malengo ni kucheza Fainali Michuanano ya Afrika

Timu ya Simba SC kupitia  Meneja Mawasiliano na habari Ahmed Ally October 1,2024  imetangaza malengo ya Msimu huu ni kuhakikisha wanarejea kucheza robo fainali katika mashimdano ya kimataifa na kuandika historia  kucheza hatua ya  nusu fainali pamoja fainali ya mashindano hayo.

" kwanza ni kuhakikisha Simba SC tunarudi kwenye robo fainali, kwakuwa tumesajili vizuri maana yake tunastahili zaidi ya robo fainali, nusu fainali pamoja na fainali ,hayo yatakuwa mafanikio ya Simba Sc ila kwasasa turudi kwenye robo fainali" amesema Ahmed Ally.
Hayo yanajiri wakati Simba SC wakitangaza rasmi kufanikiwa kunasa Saini ya mchezaji Elie Mpanzu kwa mkataba wa miaka miwili ambaye walikuwa wakimfuatilia tangu mwezi wa sita mwaka huu ila wamefanikiwa October ,2024  na tayari ameanza kuingia kwenye uwanja wa mazoezi wa Bunju Arena tayari kuungana na wachezaji wengine wa Simba SC.

"Elie Mpanzu   atakuwa nasi kwa muda huo na tutakaporidhika na ubora wake wake tutamuongezea mkataba  kutumika tena ndani ya viunga vya msimbazi kwanza bado ni kijana mdogo na uwezo wake ni mkubwa".

Simba SC  katika usajili wa dirisha kubwa msimu huu imefanikiwa kusajili wachezaji wapaya 15, wazawa sita na wakimataifa wanane na sasa imetangaza ujio wa Mpanzu mchezaji wa kimataifa DR Congo imejidhatiti kurejesha makali katika ligi ya ndani pamoja na  michezo ya kimataifa Afrika.

Mwandishi: Eunice Jacob
Mhariri:Harieth Kamugisha 

Post a Comment

0 Comments