BOT na DIB washiriki Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani

Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Bodi ya Bima ya Amana (DIB) inashiriki maonesho ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani yanayofanyika katika viwanja vya Chamanangwe kisiwani Pemba. 

Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi tarehe 10 Oktoba 2024 na mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla. 

Maonesho hayo yameanza tarehe 7 Oktoba na yanatarijwa kumalizika tarehe 20 Oktoba, 2024 yakiwa na kauli mbiu “Haki ya Chakula kwa maisha bora ya sasa na baadae”.

Mgeni Rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa ufunguzi alibainisha kwamba kwenye maadhimisho hayo watu watajionea na kujifunza kuhusu vyakula vya asili vinavyopatikana kwenye visiwa vya Pemba na Unguja sambamba na kutoa elimu ya lishe, ili kupunguza tatizo la udumavu kwenye jamii.

Afisa wa BOT Bi. Mwajabu Mntambo akitoa elimu ya alama zinazopatikana kwenye noti kwa wanafunzi


Wakati huo huo, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Shamata Shaame Khamis ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania pamoja na Bodi ya Bima ya Amana kwa kushiriki Maonesho hayo ya siku ya chakula Duniani yanayofanyika viwanja vya Chamanangwe Kisiwani Pemba 

Lengo la BOT na DIB kushiriki maonesho hayo kuwasaidia wanacnhi kutambua alama muhimu zilizopo kwenye noti, majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania pamoja na majukumu ya Bodi ya Bima ya Amana.

Waziri Shamata ametoa pongezi hizo Oktoba 10, 2024 alipotembelea banda la BOT na DIB.

Mwandishi: Ananias Khalula

Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments