Burundi yaruhusu wageni kuingia bila VISA

Rais wa jamhuri ya Burundi Mh. Evariste Ndayishimiye ametangaza rasmi kuwa kuanzia sasa, raia kutoka nchi za soko la pamoja la COMESA hawatahitaji tena VISA ili kuingia nchini Burundi.

Katika hotuba yake mapema leo katika mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa COMESA, Rais  wa Evariste Ndayishimiye, amefahamisha kuwa raia wote kutoka nchi za COMESA hawatatakiwa tena kuwa na viza watakapoingia nchini humo

Rais Ndayishimiye ameweka bayana kuwa lengo la hatua  hiyo ni kukuza umoja na utimilifu miongoni mwa nchi wanachama ili kuongeza fursa za kiuchumi.

Katika mkutano huo uliofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi, Rais Evariste Ndayishimiye,  amepewa kijiti cha uongozi na kusimamia soko la pamoja la COMESA kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia leo

Marais wa nchi za ukanda wa soko la pamoja kusini mwa Afrika (COMESA) wakishiriki mkutano wa mwaka jijini Bujumbura Burundi.

Rais wa Kenya  William Ruto amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa COMESA huku  Mh. Hakainde Hichilema Rais wa Zambia, akibaki katika nafasi ya tatu.

Evariste Ndayishimiye amezitaka nchi ambazo bado hazijatia saini mkataba wa ubadilishanaji wa biashara kufanya hivyo haraka, ili kusaidia maendeleo ya ukanda mzima wa COMESA.

Mkutano huo wa  umehudhuriwa na Rais wa Kenya, DRC, Zambia, Madagascar, Ethiopia na Rais wengine ikiwemo Tanzania wameagiza wawakilishi wao.

Mwandishi: David Ndereyimana, Bujumbura

Mhariri: Mussa Mkilanya

Post a Comment

0 Comments