Changamoto uchumi, wanawake kugombea nafasi za uongozi.


Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji,Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umewapatia mafunzo watia nia ambao tayari wamepitishwa na vyama vyao kwa  lengo la kuongeza nafasi za wanawake katika uongozi.

Afisa TGNP-Mtandao Idara ya mafunzo Anna Sangai amesema hayo Oktoba 30,mwaka huu Jijini Dar es Salaam katika semina za jinsia na Maendeleo zinazofanyika kila Jumatano.

Aidha amesema mafunzo wameyaweka mahususi kwa ajili ya kuwatia moyo kwa kuonesha juhudi za kuongeza nafasi za wanawake katika uongozi na  kwa waandishi wa habari kwa dhumuni la kuwafahamisha masuala ya jinsia ili wanapokuwa wanaandika habari zao waandike maudhui yanayo hamasisha na sio kukatisha tamaa.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa kituo Cha Taarifa na maarifa kata ya Majohe wilaya ya ubungo Tabu Ally ameeleza kuwa  changamoto kubwa inayokwamisha wanawake kupitishwa na vyama vyao katika kugombea nafasi za uongozi ni suala la uchumi.

Nae, Mwanaharakati wa Jinsia,Kennedy Anjelita ameshauri watu wote waliojiandikisha kwenda kupiga kura ili kumpata kiongozi wanaye mtaka bila kujali maamuzi yatakayotolewa baada ya kupiga kura ikiwa uchaguzi ni ni tarehe 27novemba 2024.

Mwandishi;Ellukagha kyusa.


Post a Comment

0 Comments