Mashindano hayo yamefanyika Jumapili ya Octoba 13 huko Chicago huku mwanariadha huyo akijivunia na kubainisha kuwa ni ndoto yake ya muda mrefu ya kutamani kuvunja rekodi ya Dunia nakusema amelipigania muda mrefu swala la kuwa bingwa wa Dunia kwa kuvuna rekori , wameripoti BBC
Aidha kupitia rekodi ya awali ya Tigst Assefa wa Ethiopia alikimbia karibu dakika mbili na zaidi huku ikibainishwa kuwa Chepngetich ndiye mwanamke wa kwanza kukimbia marathon chini ya saa mbili na dakika 10 ingawa awali Assefa aliweka rekodi kwa ushindi wa Berlin Marathon 2023 kwa saa mbili, dakika 11 na sekunde 53.
Katika hatua nyingine Kinyang’anyiro za mbio za wanaume Mkenya John Korir alikimbia muda wake binafsi na kujinyakulia ushindi wa kabla huku akitoa heshima kwa mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia Kelvin Kiptum raia kutoka nchini Kenya ambaye alishinda rekodi hiyo mwaka jana.
Kiptun aliweka rekodi ya sasa ya Dunia ya kukimbia saa mbili na sekunde 35 mjini Chicago miezi minne kabla hajafariki Dunia akiwa na umri wa miaka 24 kwa ajali ya gari huku Kariro alisema alitumia rekodi ya mwenzake kama hamasa ya kufanya vizuri siku ya Jumapili.
Mashindaano hayo riadha za marathon yamewaweka wakenya katika nafasi nzuri kidunia ya kufanya vizuri katika mashindano hayo ambao ni Ruth Chepngetich aliyevunja rekodi ya dunia kwa upende wa wanawake, John Korir aliyeshika nafasi ya kwanza kwa wanaume, mwingine ni Amos Kipruto aliyemaliza nafasi ya tatu na kuwafanya kuwa wakenya wanne kati ya watano waliofanya vizuri katika Riadha.
Ifahamike kuwa ushindi wa mwanamama Chepngetich ni wa tatu kwake huko Chicago, ambapo alishindwa kuvunja rekodi ya Dunia 2022 ambapo mkenya mwenzake Brigid Kosgei alimshinda kwa sekunde 14, mashindano manne ya mbio za Marathon kati ya matano ya kasi zaidi ya wanawake yamekuwa yakifanyika Chicago katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Mwandishi; Sharifat Shinji
Mhariri; Ramadhani Zaidy
0 Comments