Timu ya Tanzania Taifa Stars yakubali kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) katika michuano ya kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON 2025 nchini morocco.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Dar es Salam Octoba 15, 2024 majira ya saa 10:00 jioni masaa ya Afrika mashariki huku Tanzania Taifa Stars ikibanwa mbavu kwa mabao yaliyofungwa kipindi cha pili na Meshack Elia mnamo dakika ya 87 na 90+3 na kufanya mchezo utamatike kwa Tanzania kupoteza kwa magoli 2-0.
Baada ya mchezo huo timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefuzu kwenda AFCON 2025 kufuatia ushindi huo huku Tanzania ikisaliwa na michezo miwili mkononi kati ya Ethiopia utakaochezwa nchini Ethiopia pamoja na Guinea utakaochezwa Katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salam.
Taifa Stars inasalia nafasi ya pili ikiwa na alama nne baada ya mechi nne huku Guinea ambayo imecheza mechi tatu ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu wakati Washika mkia Ethiopia wakiwa na alama moja baada ya mechi tatu hata hivyo DR Congo ikiongoza kundi kwa alama 12 na kuifanya ufuzu moja kwa moja.
Mwandishi; Sharfat Shinji
Muhariri; Ramadhan Zaidy
0 Comments