*Wananchi,Wanasiasa waonywa kupotosha wanajamii kutojiandikisha.
Summary:Mkuu wa wilaya Bukoba Erasto Sima amehimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura huku akiwaonya wananchi wajiandikishe kwenye Daftari maana Kitambulisho cha mpiga kura hakitahusika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Bukoba.Mkuu wa wilaya Bukoba Mkoa Kagera,Erasto Sima amewataka wananchi na wanasiasa kuacha tabia ya kupotosha jamii kuwa kitambulisho cha mpiga kura kitahusika kwenye uchaguzi serikali za mitaa huku akihimiza wajiandikisha kwenye daftari kupata haki ya kumchagua kiongozi wampendae Novemba,2024
Manispaa ya Bukoba inakadilia kuandikisha wanananchi wapiga kura serikali za mitaa mwaka huu 2024 wapatao 87,647 kiwa wanaume ni 40,870 wanawake 47,777 kutoka katika Mitaa 66 yenye vituo 84 vitakavyotumika.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura serikali za mitaa Leo Ijumaa Octoba 11,2024,Mkuu huyo wa wilaya Bukoba Erasto Sima amewataka viongozi wa vyama vya siasa na wananchi kuacha tabia ya kupotosha jamii kuwa Kitambulisho cha mpiga kura kitatumika kwenye uchaguzi ili wasiende kujiandikisha tena.
"Nawaonya wananchi na wanasiasa mbali mbali mtu yoyote asimdanganye Mwenzake kuwa ata asipokwenda kujiandikisha ana Kadi ya mpiga kura huo niongo jitokezeni kwa wingi kwenye mitaa yenu jiandikisheni sisi wenyewe tayari asubuhi tulifanya hivyo"amesema
Afisa Uchaguzi Manispaa ya Bukoba,Erick Bozompora amesema vituo vyote 82 katika mitaa hiyo wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujiandikisha na hatua za kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa maandalizi na vifaa vikotayari walishavipokea.
"Niwajibu sasa wa kila mwananchi kujiandikisha kwa ajili ya kupata haki ya kuwa kwenye orodha ya wapiga kura katika manispaa hii vifaa viko tayari nasisi tuko tayari wananchi wanazidi kuonesha mwiitikio mkubwa"amesema
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM),mkoa Kagera,Nazir Karamagi ameshiriki zoezi la kujiandikisha katika kituo cha kujiandiksha cha Hamugembe manispaa ya bukoba huku akiwataka wananchi kuhamasishana kwenda kwenye vituo vya kujiandikisha huku akiwataka wanajamii kuwasaidia wasiyojiweza kusaidiwa kuwapeleka kwenye vituo ili wajiandikishe pia.
"Niombe tuwasaidie wenzetu kwenye zoezi hili ili nawao wapate nafasi na sifa za kushiriki uchaguzi huu wa serikali za mitaa"amesema
Uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utafanyika Novemba 27 Mwaka huu katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa.
Mwandishi: Ananias Khalula, Bukoba
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments