FDC Kigamboni washukuru Waziri Mkuu kutumia Chuo hicho kikazi

Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC) Kigamboni kinaishukuru ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila kwa kutumia Chuo hicho kumpokea na kuzungumza ba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Shukurani hizo zimetolewa na Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Ramadhani Simba wakati akizungumza na Buha News muda mfupi baada ya Waziri kuu kukamilisha kikao kazi cha viongozi mbalimbali wa serikali katika wilaya ya Kigamboni

Mhandisi Simba amebainisha kuwa ujio wa Waziri mkuu katika Chuo hicho kumekitangaza chuo hicho kwa umma na watalaam kutokana na fursa zilizopo chuoni hapo

"Kwakweli Kigamboni FDC tumefurahi sana halmashauri kuona kuwa ukumbi wetu unastahili kutumiwa na Waziri mkuu, nitoe wito kwa taasisi nyingine na wadau wa maendeleo kukitumia chuo chetu kwa shughuli za kijamii na kitaaluma" Amesisitiza Mhandisi Simba.



Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe Kassim Majaliwa leo  tarehe 6/10/2024 alizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya kigamboni katika ukumbi  wa chuo cha maendeleo  ya wananchi KIGAMBONI ambapo mazungumzo hayo yalihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwepo mkuu wa mkoa wa DSM  Mhe. Albert Chalamila

Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na katibu  tawala wa mkoa wa DSM sambamba na wenyeji wake mhe. Halima bulembo- mkuu wa wilaya ya  Kigamboni, mkurugenzi wa manispaa ya kigamboni, na mbunge  wa kigamboni ambaye pia ni mkurugenzi wa WHO ukanda wa Afrika mhe. Dr. Faustine Ndugulile 

Katika mkutano huo Waziri mkuu kassim majaliwa alitoa agizo kwa mamlaka za sheria kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi ikiwepo ubadhilifu wa mali za umma na ukwamishaji wa miradi ya maendeleo.

Post a Comment

0 Comments