Kamala Harris ametumia kile kilichoitwa 'hotuba yake kuu ya mwisho katika kampeni zake' kwa kuwakumbusha Wamarekani jinsi maisha yalivyokuwa chini ya Donald Trump.
Amewapa wapiga kura njia tofauti ya kusonga mbele Akizungumza mbele ya umati mkubwa uliofurika katika bustani iliyoko karibu na Ikulu ya White House na Mnara wa Washington, Harris amesema atawasikiliza Wamarekani wakati wote hata kama hawatompigia kura.
Harris akizungumza katika bustani ya ikulu karibu na white house Picha: SAUL LOEB/AFP
Alichagua eneo hilo la mjini Washington DC kwa sababu ndilo ambalo Mrepublican Trump alitumia kuuchochea umati uliovamia Jengo la Bunge mnamo Januari 6, 2021.
akiongeza kuwa rais huyo wa
zamani anataka kurejea Ikulu ya White House sio kuyaangazia matatizo yao bali
matatizo yake.
"Tunamfahamu Donald
Trump ni nani," Alisema Harris, akiongeza kuwa rais huyo wa zamani
"alilituma kundi la watu wenye silaha” kulivamia bunge la Marekani katika
jaribio la kuyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020.
Alijionesha kuwa kama mtetezi mwenye nguvu wa haki za wanawake,
binti ambaye alifanikiwa maishani kupitia bidii bila msaada wa mali, na mtu
aliyekubaliana na hali halisi ya mambo nchini humo. Ikiwa hii itatosha katika
kinyang'anyiro kikali cha kuwashawishi wapiga kura ambao hawajaamua katika
mwaka huu wa uchaguzi ambao haujawahi kushuhudiwa bado haijabainika.
Mkutano huo wa kampeni uliojiri wiki moja tu kabla ya Siku ya
Uchaguzi (Novemba 5), ulihudhuriwa na watu 75,000, kulingana na waandalizi.
Idadi hiyo haikuweza kuthibitishwa maramoja.
Mwandishi :Abel Mahenge
mhariri :Ellukaga Kyusa
0 Comments