Shambulio hilo limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 14,2024 kaskazini mwa Israel huku jeshi hilo likiongeza kuwa wanajeshi saba wamejeruhiwa vibaya katika shambulio hilo kwenye kambi ya Binyamina mji ulioko umbali wa maili 20 (33km) kusini mwa Haifa.
Kundi la jeshi la Hezbollah limedai kuhusika na shambulio hilo ambalo ilisema liliilenga kambi ya mafunzo ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Brigedi ya Golani katika eneo hilo lenye makao yake makuu kati ya Tel Aviv na Haifa.
Ofisi ya vyombo vya habari vya kundi la kijeshi la Hezbollah limeripoti kuwa shambulio hilo lilikuwa ni kujibu mashambulizi ya Israel kusini mwa Lebanon na Beirut lililofanyika siku ya Alhamisi.
Awali wizara ya mambo ya nje ililiomba baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kutowa azimio la kutaka usitishaji kamili wa vita na kwamba serikali yake inaendelea kuliunga mkono azimio nambari 1701 lililopitishwa mwaka 2006.
Mwandishi; Ramadhani Zaidy
0 Comments