
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa nchi
yake imepanga kulipa Kisasai Iran, kutokana na
mashambulizi yaliyofanywa na nchi hiyo mwanzoni mwa juma hili.
Netanyahu amesema hayo Octoba 2,2024 nchini Israel na kusema
kuwa kinachofanywa na iran kuishambulia Israel ni kitendo kikubwa cha uchokozi
na iwapo Iran haitozuiliwa basi wimbi jengine la makombora halitoilenga tu
Israel bali mataifa mengine pia.
Kwa upande wa Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameionya na kutishia
kuwa Iran itajibu vikali zaidi, iwapo Israel itathubutu kufanya mashambulizi ya
kulipiza kisasi cha mashambulizi hayo.
Naye Rais wa Marekani Joe Biden ambae ndiye mshirika mkubwa
wa Israel siku ya Jumatano alisema kuwa
hatoiunga mkono Israel iwapo itashambulia miundombinu ya zana za nyuklia za
Iran.
Iran ndiye mdhamini mkuu wa makundi ya Hamas Pamoja na
Hezbollah Ambayo ni msingi wa mgogoro huo, huku Umoja wa Mataifa ukiripoti
kuwa Iran imetuma makombora karibu 200
Israel ili kuizuia Israel kutoendelea na
mashambulizi yake .
Mwandishi :Ramadhani Zaidy
Mhariri: Harieth Kamugisha
0 Comments