Kasulu yagundua njia mpya uchaguzi wa serikali za mitaa


Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Izack Antony Mwakisu amehimiza wananchi kundelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftrari la mpiga kura ili kukidhi vigezo na sifa ya kuchagua viongozi wa serikali za mitaa.

Ameyasema hayo wakati wa bonanza la uzinduzi wa kujiandikisha katika daftari la mpiga kura lililofanyika katika uwanja wa Umoja na kusema kuwa haki na mafanikio yanapatikana kwa kujitokeza kujiandikisha ili kupata sifa ya kuwa mwananchi mwenye haki ya kumchagua kiongozi.

"Bonanza hili limefanya tufurahi kwa pamoja linasadifu uwajibikaji wa kila mmoja kujitokeza katika kujiandikisha ili kupata kiongozi sahihi, Haki yako ni kupata kiongozi uliyemkusudia kukuongoza kwa miaka mitano" amesema Kanali Izack Antony.


Mkuu wa wilaya ya kasulu Kanali Izack Antony (katikakati) katika bonanza la kuhamasisha uandikishaji wa daftari la mpiga kura.

Aidha Kanali Izack Antony ameongeza kuwa kila mwananchi pamoja na viongozi wao wanapaswa kushirikiana kikamilifu ili kuelimisha jamii hasa wale waliofika miaka kumi na nane waweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya kasulu Bi. Teresia Mtewele amesema kuwa serikali imetenga vituo 225 vya kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili kurahisisha zoezi la uandikishaji katika wilaaya ya Kasulu.

"Nimefurahi kuwaona wananchi na wafanyakazi wa halimshauri zote za kasulu , lengo kuu ni kuhamasisha wananchi kutambua wajibu wa kila mwanchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kupata kiongozi atakaeleta maendeleo katika mitaa yetu" Amesema Teresia Mtewele.

Bonanza hilo likiwa la kwanza wilayani kasulu kufanyika chini ya uongozi wa Kanali Izack Antony Mwakisu likihusisha michezo mbalimbali ikiwemo waimbaji binafsi, mashindano ya mpira wa miguu kwa wasichana lengo likiwa kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mwandishi; Abel Mahenge

Mhariri; Ramadhani Zaidy

Post a Comment

0 Comments