Kocha Étienne Ndayiragije asimamishwa kazi

Shirikisho la soka nchini Burundi FFB limemsimamisha kazi mkufunzi wa timu ya taifa hilo maarufu INTAMBA MU RUGAMBA kufuatia kugubikwa na matokeo mabaya katika mashindano ya kimataifa

Habari kutoka nchini katika shirikisho hilo zilizotolewa mapema leo jijini Bujumbura zinafafanua kuwa uamuzi ambao umechukuliwa baada ya kufanyika  makubaliano ya pande zote mbili.

Etienne Ndayiragije amekuwa akishutumiwa na mashabiki pamoja ba baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa kuwa anaacha kwa makusudi  kuweka kwenye list wachezaji wa kimataifa na walio na uzoefu na  kupelekea kupata matokeo mabaya.

Duru za Soka nchini Burundi zinaeleza kuwa kutokana na tabia hiyo ya kibaguzi dhidi ya wachezaji wanaokipiga nje ya hichi hiyo, wachezaji wengine waliapa kutorudi kwenye kikosi mpaka pale kocha Étienne atakapoondolewa.

Mkataba wa Ndayiragije wa kuinoa timu ya taifa la Burundi ungemalizika mapema mwezi  Januari 2025, hata hivyo maamuzi ya FFB huenda yakapelekea kutimuliwa kabisa kikosini.

Burundi yenye wachezaji wengi wa kimataifa na idadi kubwa ya makocha katika nchini za afrika mashariki imeondoka ikiwa na alama 3 pekee katika mashindano ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON.

Ndayiragije amewahi kufundisha timu kadhaa za Tanzania ikiwemo Mbao FC, Azam, Geita Gold na timu ya Taifa ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments