Mahakama ya nchini Kenya yatoa msimamo juu ya Sheria ya Fedha .



Mahakama ya Juu nchini Kenya imeubatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa ukiifuta sheria ya fedha ya mwaka wa 2023. Maandamano makali mwezi Juni na Julai ya kupinga sheria hiyo yalisababisha vifo vya watu 60.

Hatua hiyo ni ushindi kwa serikali baada ya maandamano yaliyomlazimu Rais William Ruto kuondoa mswada wa fedha wa mwaka huu. Mahakama ya Juu imesema katika uamuzi wake kuwa imeuweka kando uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulioitangaza Sheria yote ya Fedha ya 2023 kuwa kinyume na katiba.

Serikali ya Ruto, iliyoingia madarakani Septemba 2022, ilitaka kuweka awamu mpya ya nyongeza ya kodi mwaka huu. Hatua hiyo iliwakasirisha raia wengi na kusababisha maandamano makali mwezi Juni na Julaiambapo zaidi ya watu 60 waliuawa.

Ruto anahoji kuwa nyongeza ya kodi ni muhimu kusaidia kufadhili miradi ya maendeleo nchini Kenya na kulipia mzigo mkubwa wa deni la umma.

Ikumbukwe kuwa Rais ruto aliingia madarakani baada ya  uchaguzi wa Kenya tarehe 9 Agosti 2022 Ruto alitangazwa kuwa mshindi tarehe 15 Agosti 2022 Matokeo yaliyotangazwa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na mipaka nchini Kenya Wafula Chebukati yalikanushwa na makamishna 4 wa Tume Huru ya Uchaguzi Mpinzani wake Raila Amolo Odinga alikataa matokeo hayo na kuwasilisha kesi kwenye mahakama ya juu ya Kenya Hata hivyo uamuzi ulithibitisha uhalali wa matokeo yaliyotangazwa awali.

Mwandishi : Abel  Mahenge 

Mhariri :Ellukaga kyusa 




Post a Comment

0 Comments