Mamilioni ya watu kusini mwa afrika kukubwa na baa la njaa

Shirika la Mpango wa chakula la umoja wa mataifa WFP limesema kuwa mamilioni ya watu wanaoishi kusini mwa Afrika wanakabiliwa na baa njaa kutokana na ukame wa kihistoria unaozikumba nchi hizo.

WFP imetoa taarifa hiyo usiku wa kumamkia Octoba 16, 2024 na kuonya kuwa ukame huo wa kihistoria unatishia kusababisha maafa ya makubwa ya kibinaadamu katika nchi za kusini mwa afrika.

Kwa upande wa msemaji wa WFP katika eneo la kusini mwa Afrika Tomson Phiri amesema kuwa Takribani watu milioni 27 wameadhirika na ukame huwo huku zaidi ya watoto Milioni 21 wakiwa na utapialo kutokana na ukosefu wa chakula.

Phiri ameongeza kuwa WFP inasambaza chakula na kusaidia mipango ya misaada huku ikiwa imepokea karibu dola milioni 73.8 kati ya dola milioni 369 inazohitaji kwa ajili ya msaada wa chakula katika nchini hizo.


Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP)

Kwa mujibu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ina nchi 16 ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Comoro, DRC, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Seychelles, Tanzania, Zambia, Zimbabwe kati ya hizo Nchi tano ambazo ni Lesotho, Malawi, Namibia, Zambia, na Zimbabwe imetangaza hali ya janga la kitaifa katika muda wa miezi iliyopita kwasababu ukame huo umeharibu mazao na kuangamiza mifugo.

Mwandishi; Ramadhan Zaidy

Post a Comment

0 Comments