Kumeripotiwa mapambano makali huko mashariki mwa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo bahina ya M23 Na wazalendo wanaloisaidia Jeshi la taifa hilo.
Mapambano hayo yalianza alfajiri ya Jumapili ya tarehe Oktoba 20, 2024
Wakati M23 wanaosaidiwa Na RDF Jeshi la Rwanda wakishirikiana Na AFC , Corneille Nanga ambao Walishambulia Kijiji cha Kalembe Wilayani Walikale kwenye Mikoa wa Kivu ya kaskazini.
Mapambano hayo yametokea wakati Jeshi la serkali laendelea kutekeleza makubaliano ya usitishwaji vitæ kama walivyo hafikiana kwenye kikao vya Angola;
Kati ya ujumbe wa serkali ya Rwanda Na ule wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo chini ya rais wa Angola Joao Lorenzo.
Hali hiyo imawapelekea wapiganaji wa M23 Na washirika wao kuelekea.delza kushika karibia mitaa yote , Wilaya zote za mkoa wa Kivu ya kaskazini ,na kutokana na hali hiyo waziri mstahafu Pia mbunge wa taifa wa maeneo hayo Bw Willy Mishiki;
ameeleza kukerwa na hali hiyo .
"Ndugu manaibu wenzangu wa kitaifa, vita vya Mashariki vimechukua mkondo wa mwisho leo na kuanguka kwa mtaa wa Kalembe Jumapili hii tarehe Oktoba 20/2024 saa Tatu kabla ya adhuhuri kumeleta mshutuko " alisema Mbunge huyo .
Hicho ni kijiji cha kwanza kufikiwa na wavamizi M23/RDFkwenye eneo hilo la Walikale;
Ambacho kilikuwa ni kizuizi cha mwisho kwa adui Hao kufika kwenye Mikoa ya Tshopo, Kivu Kusini na Maniema ambayo ni mlango wa mwisho kuelekea majimbo mengine ya nchi.
Mapigano hayo yalianza saa kumi algajiri jumapili wakati wavamizi hao waliposhambulia maeneo ya Wazalendo wa RAD vikundi vya NDC renove na APCLS ambao kwa muda wa miezi 2 walikuwa wakilalama na kudai kwamba risasi Zimewaishia kutoka kwa washirika wao FARDC Jeshi la taifa.
Mbunge huyo ameomba kuitishwa kikao cha dharura kuhusu suala hili la usalama wa kibinadamu kabla ya kuchelewa Kwa kuwa hali ya kuzingirwa kwa Mikoa ao État de Siège na kumepoteza udhibiti wa karibia wilaya 6 za mkoa wa Kivu ya Kaskazini uliovamiwa na M23 na ADF huku jiji la Goma pekee likiwa linamebaki japo nalo linazungukwa na M23 na Jeshi la Rwanda
Mwandishi : Mseke DIDE kutoka Beni.
Mhariri: Harieth Kamugisha
0 Comments