Mbaloni kwa kujeruhi na kutishia silaha

 


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Derick Derick Junior mkazi wa Salasala Kinondoni kwa tuhuma za kujeruhi na kutishia kwa silaha.

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 28, 2024 na kamanda wa polisi wa kanda hiyo, Murilo Jumanne Murilo imesema kuwa baada ya uchunguzi wa tukio hilo lililotokea Oktoba 27, saa 12: 30 asubuhi maeneo ya Masaki, mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru kwa kumpiga na kitako cha bastola na kumjeruhi jicho na pua.

Katika taarifa yake, Kamanda Murilo amesema Julian Bujuru anaendelea vizuri na matibabu.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa  katila vyombo vingine vya sharia haraka iwezekanavyo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments