Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 17, 2024 Jijini Dodoma alipokutana na Uongozi wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania (TANNA) na kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa hoja za wauguzi zilizo jitokeza wakati wa mkutano wa mwaka uliofanyika Mei, 12, 2024 kwa lengo la kuongeza ubora wa huduma za Afya.
Mhe. Mhagama ameongeza kuwa anatambua mchango na kazi kubwa ya wauguzi na wakunga katika sekta ya afya na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuhudumia wananchi katika sekta hiyo .
“Wakati tunafanyia kazi changamoto zenu tusaidieni kusimamia maadli kwa wauguzi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi" amesema Mhe.Mhagama
Kwa upande wake rais wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania ( TANNA), Alexender Baluhya amesema kuwa wauguzi na wakunga wanaimani na serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa ni sikivu na itatatua changamoto zao kwa wakati ili kuleta tija katika utendaji kazi wao
Lengo la Mkutano huo wa Mhe. Mhagama na Uiongozi wa wauguzi na wakunga ni kufatilia utekelezaji wa hoja zilizotolewa katika mkutano wa mwaka uliofanyika pale Mkoani Tanga na moja ya hoja zilizotolewa ni pamoja na kuomba kupandishwa madaraja kama ilivyo kwa kada nyingine
Mwandishi: Harieth Kamugisha
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments