Leo Tanzania inaadhimisha miaka 25 bila Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliheshimiwa na kupewa hadhi ya Baba wa taifa.
Maadhimisho hayo yanafanyika jijini Mwanza yakiambatana na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na wiki ya vijana ambayo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 14, 2024 ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Kumbukizi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mt. Francis Xavier Nyakahoja.
Katika Ibada hiyo Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wamehudhuria akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, Jijini Mwanza.
Pamoja na mambo mengine Tanzania inamkumbuka Nyerere na vita vya Kagera ambayo viliiacha nchi hiyo katika dhiki kubwa na umaskini
Wazee walioshiriki vita hivyo wanaitazamaje kuhusu Nyerere na vita dhidi ya Idd Amini? Na wanaionaje Tanzania bila Nyerere.
Maswali mengi yamekuwa yakiulizwa na watanzania wengi ikiwemo Je? Tanzania bado ina viongozi wa Kariba ya Nyerere wanaojitoa Kwa ajili ya taifa?
Swali la pili ni kwamba wakati wa vita vya Kagera kulikuwa na mwamko wa vijana ikitokea mstari wa Mabele vitani, je Leo ikitokea msukomsuko kama huo bado wapo watanzania watakaojitoa?
Mzee Pius Ngeze aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera wakati wa Vita vya Kagera anamuona Mwalimu Nyerere kama kiongozi wa aina Yake aliyezaliwa na uongozi ndani yake na anakiri kwamba huenda wapo viongozi wazalendo lakini hawezi kuwepo Nyerere mwingine
Mzee Ngeze anamsifu Nyerere Kwa kujenga taifa moja na kuondoa dhana ya ukabila, ukanda na lugha kwa kuhamasisha na kifundisha lugha ya Kiswahili kama lugha ya taifa
Anakiri kuwa kama siyo misimamo ya Nyerere kusingekuwepo na muungano na nchi ingekuwa kama nchi za jirani ambayo baadhi yake hazina lugha ya taifa na kila kabila hutumia lugha asilia huku lugha za kigeni kama vile Kifaransa, Kigereza na Kireno zikitumika kama lugha za taifa.
Kuhusu vita vya Kagera Mzee Ngeze anamsifu Nyerere kwa uamuzi wake wa Busara wa kumpiga na kuondoa Madarakani Idd Amini Dada akitaja kuwa uamuzi huo haukuikomboa ardhi ya Tanzania eneo la Kagera pekee Bali pia vilikiwa ni vita vya kuikomboa Uganda.
Mwandishi: Prosper Kwigize
kwigizebaraka@gmail.com
0 Comments