Vijana watakiwa kujitokeza kuwania uongozi serikali za mitaa

 

                                                Picha :Michuzi blog

Mkuu wa Idara ya Vijana Hamasa SMAUJATA Mkoa wa Tanga Bw. Athumani Sheria amewataka vijana wanajitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwa mchango wao kwenye maeneo yao unaweza kuwa na tija kubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo yamitaa.

Wito huo umetolewa leo wakati akizungumza na umoja wa vijana mkoaniTanga (SMAUJATA) na kueleza kuwavijana Mkoani humo wanatakiwa kuhakikisha wanawachagua viongozi  ambao watakuwa ni sauti ya wananchi kwenye maeneo yao na sio wachumiatumbo wakati wa uchaguzi wa Serikali zaMitaa unao tarajiwa kufanyika Novemba 27mwaka huu .

"Ndugu zangu vijana katika uchaguzi waSerikali za Mitaa tuhakikishe tunatumia haki yetu ya msingi ya kuwachagua viongozi  ambao watakuwa sauti ya wananchi kwakuchochea maendeleo na sio kutafuta kipato chao  wajali zaidi kutimiza ahadi zao nakuangalia maslahi ya wananchi"  AlisemaSheria

Aidha wamemshukuru Rais Dkt SamiaSuluhu kwa uwekezaji wa Bilioni 429. katika Bandari ya Tanga ambayo kumewezesha maboresho makubwa na hivyo kuufungua kiuchumi mkoa huo nakuongeza kuwa maboresho hayo yamewasaidia kupata ajira lakini Serikali kuongeza pato pamoja na kuwainua kiuchumi vijana wa bodaboda na mamalishe pamoja na wafanya biashara mbalimbali mkoani humo.

Mwandishi ;Ellukagha Kyusa

Mhariri  : Abel mahenge 

Post a Comment

0 Comments