Polisi ahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.



Polisi ajulikanae kwa jina la Ndayisaba Leonidas amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani,kutoruhusiwa kumiliki silaha, kutorejea kazini pamoja na kulipa fidia ya milioni 175 pesa ya Burundi kwa familia za marehemu baada kukutwa na hatia ya kuuwa raia kwa makusudi.

Muendesha mashtaka kwenye Mahakama kuu ya Taifa ya mkoa wa Ngozi magharibi mwa Burundi Akisoma kesi hiyo Oct 28, 2024 amesema kuwa afisa huyo wa  polisi anashtakiwa   kwa kuua watu watatu  kitendo  alichokifanya Jumamosi ya 26 0ct 2024 majira ya satatu usiku kwenye baa ilioko mjini Ngozi  polisi huyo aliwafyatulia risasi watumishi  wawili na mteja mmoja wote wakafariki papo kwa hapo.

Polisi huyo amejitetea mbele ya mahakama  akidai kuwa aliwaua watu hao kwa sababu walikuwa wakimshambulia na pia wakijaribu kumnyang’anya silaha, lakini hoja yake imetupiliwa mbali na mahakama hiyo.

 Mwandishi:David Ndereyimana.

Muhariri: Eunice Jacob.

Post a Comment

0 Comments