|
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameziagiza taasisi zinazosimamia masoko mapya kuweka Viwango vidogo vya malipo kwa Wafanyabiashara na Wajasiriamali ili wamudu kulipa na kuendelea na biashara katika mazingira mazuri.
Dk,Mwinyi ameyasema hayo Oktoba 27 2024 alipofungua soko jipya la kisasa la Jumbi, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dk, Mwinyi amewahakikishia Wafanyabiashara kuwa Serikali itaendelea kuwaandalia mazingira Bora zaidi sokoni hapo yatakayoendana na soko hilo.
Aidha Dk, Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali imetenga kiasi cha shillingi Bilioni Mia moja kwa ajili ya kuwapatia mitaji Wajasiriamali na Wafanyabiashara kuimarisha Biashara zao na kuwataka Wajasiriamali ambao bado hawajapata mitaji kujipanga vema katika Vikundi ili Serikali iwapatie mitaji hiyo .
WATANO KUTOKA KULIA NI RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI MHE. DK HUSSEIN ALI MWINYI NJE YA JENGO LA SOKO JUMBI MKOA WA MJINI MAGHARIBI
Dk, Mwinyi ameagiza soko kuwa wazi Usiku na mchana wafanyabishara kuruhusiwa kufanya shughuli zao muda wote ili kuongeza mapato .
Sanjari na hayo Dk Ali,Mwinyi amewaahidi wananchi kuwa ataendelea kujipambanua kwa Vitendo kutimiza ahadi alizoziahidi wakati wa Kampeni mwaka 2020.
Mwandishi : Eunice Jacobo
Mhariri : Abel Mahenge
ReplyForward |
0 Comments