RC Kagera uso kwa uso na TRA, mkakati mpya wa kodi waja

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Fatma Mwasa leo tarehe 17/10/2024 amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalum wa kodi kutoka Mmlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano, ikiongozwa na Meneja wa Mkoa wa Kagera TRA Bw. Castro John. 

Timu hii ya Maafisa kodi wapo Mkoani Kagera kwa kwa ajili ya kutekeleza kampeni Mlango kwa Mlango (Door to Door) yenye lengo la kuwafuata walipakodi sehemu zao za biashara na kutoa elimu ya kodi, kuwakumbusha wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi kwa wakati na hiari, na kusikiliza changamoto mbalimbali za kikodi wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza jukumu lao la kulipa kodi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, ameipongeza TRA kwa kuendelea kuwa karibu na walipakodi na kutoa elimu stahiki, na kwamba inachagiza ulipaji wingi wa kodi na kusaidia serikali kuwahudumia wananchi katika huduma za kijamii, kama vile uimarishaji wa miundombinu, sekta ya afya elimu na usafirishaji. 

Amewataka walipakodi mkoani Kagera kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kulipa kodi kwa wakati na kukumbuka kutoa risiti za kielektroniki (EFD) kila wanapofanya mauzo na kudaai kila wanapofanya manunuzi kwa kuwa hili ni takwa la kisheria kwa maendeleo ya taifa letu. 

Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Kagera, amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa ushirikiano na maelekezo yake katika kuimarisha mazingira ya ukusanyaji wa kodi mkoa wa Kagera.

Zoezi la utoaji wa elimu ya kodi Mlango kwa Mlango linaendelea katika wilaya ya Bukoba.

Post a Comment

0 Comments